Kijiji cha Naruora kiko mashariki mwa nchi ya Uganda eneo la Alale, kimezingirwa na milima, ndani mwake kuna shughuli inayoendelea, ya uchimbaji dhahabu, kuna umri wa aina yote, wapo wanawake wajawazito, waliowafunga watoto migongoni ili kurahisisha shughuli ya kusafisha dhahabu, vijana, wazee na hata watoto.